Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa amefungwa mguu kwa kutumia nyaya ya umeme na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess ikiwa ni mfano jinsi wanyamapori wanavyonaswa katika mitego ambayo imekuwa ikitegwa na majangili kwa ajili ya kuuwa wanyamapori kwa ajili ya kujipatia kitoweo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess wakiwa wameshika baadhi ya nyama za umeme 30 ambazo zimeteguliwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ambazo kama zisingeteguliwa zingeweza kuuawa wanyamapori wapatao 380.Ametaja wanyamapori hao waliokutwa wamekufa kuwa ni twiga moja pamoja na swala wawili hata hivyo Dkt. Ndumbaro amesema kupitia mradi huo wa kunasua mitego Wizara hiyo imekuja na mbinu ya kuwashirikisha wanavijiji wanaopakana na Hifadhi kwa ajili kupambana na majangili hao.
Akizungumzia aina mpya hiyo ya ujangili, Dkt. Ndumbaro amesema majangili hao wamekuwa wakitega mitego hiyo kwa ajili ya kuwanasa wanyapori kwa ajiili ya kujipatia nyama ya kula.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa kikosi maalum cha kutegua mitego ilitegwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Wengine ni baadhi ya ujumbe kutoka Balozi wa Ujerumani nchin Tanzania pamoja na Watumishi wa Hifadhi ya Nyerere. Amefafanua kuwa baadhi ya Jamii zimekuwa zikiendeleza imani potofu ya kula nyamapori kwa kuamini kuwa ndo nyama bora kupita zote kuwa hali imekuwa ikichangia ujangili kwa ajili ya kitoweo.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mhe. Regine Hess amesema Serikali yake iliamua kufadhili mradi wa kutegua mitego hiyo baada ya Serikali ya Tanzania kufanikisha kukomesha ujangili kwa asilimia 90 hususan ujangili wa biashara.
Mhe. Hess ameleezea kuwa mradi huo pia umeonesha mafanikio makubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo mitego mingi imeweza kuteguliwa.
Aidha, Balozi huyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kuwa Serikali ya kwanza Barani Afrika kwa kusimamia shughuli za uhifadhi kiukamilifu.