Wizara zapokea mkakati wa pamoja kuendeleza michezo nchini

NA MWANDISHI MAALUM

TIMU ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ulinzi na Mambo ya Ndani, Novemba 19, 2021jijini Dodoma imepokea mpango mkakati wa pamoja wa jinsi ya kuendeleza michezo nchini na mpango mkakati wa muda mfupi wa kuandaa Timu za Taifa kushinda kwenye mashindano ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya madola yatakayofanyika nchini Uingereza Julai 2022.
Timu ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ulinzi na Mambo ya Ndani, Novemba 19, 2021 jijini Dodoma imepokea mpango mkakati wa pamoja wa jinsi ya kuendeleza michezo nchini na mpango mkakati wa muda mfupi wa kuandaa Timu za Taifa kushinda kwenye mashindano ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya madola yatakayofanyika nchini Uingereza Julai 2022.

Mipango hiyo imewasilishwa na Kamati maalum inayojumuisha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (WUSM), Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)iliyoundwa kufuatia maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ya kutaka vyombo hivyo vya Michezo kuchukua hatua za kuimarisha Michezo ili kuleta mafanikio kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Ikiwasilisha taarifa hiyo ya mipango Kamati hiyo ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Michezo linalojumuisha vyombo mbalimbali vya dola nchini ilieleza kuwa mipango hiyo imekuja na mkakati mahususi ili kutumia vipaji vilivyoko katika vyombo hivyo kusaidia Timu mbalimbali za Taifa.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo, amesema vijana wengi walioko kwenye majeshi nchini wanavipaji ambavyo bila kuweka mikakati hawatapata nafasi ya kuisaidia nchi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya kuandaa Mpango Mkakati wa pamoja wa WUSM, BMT na BAMMATA, Kanali Erasmus Bwegoge

ambaye pia ni Mwenyekiti wa michezo Kanda ya JKT amesema mkakati wa mipango hiyo imepambanua kikamilifu malengo, majukumu, mikakati, shabaha, na viashiria vya mafanikio na umetoa mwelekeo wa hatua mbalimbali zitakazochukuliwa na wadau wote ili kufikia lengo la Mhe. Rais la kufanya vizuri katika Michezo kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news