Ajali iliyohusisha basi la Classic kutoka Dar-Congo, malori yaua na kujeruhi usiku wa leo

NA MWANDISHI MAALUM

WATU kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha malori matatu na basi la abiria ambayo imetokea usiku wa leo wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.
Ajali hiyo ambayo imetokea katika mji wa Mlowo wilayani humo, basi ambalo limeteketea kwa moto limefahamika kwa jina la Classic ambalo lina namba za usajili 68842 AK 05 linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, basi hilo lilikuwa limetoka jijini Dar es Salaam kuelekea Tunduma kabla ya kuvuka kuelekea nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
 
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Omary Mgumba ameeleza katika eneo la tukio muda mfupi uliopita kuwa,basi la Classic lilikuwa na abiria 13 na sita ni wafanyakazi wa basi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba (kushoto) akiwa na Katibu Tawala Mkoa,Missaile Albano Musa eneo la ajali Mlowo.

RC Mgumba ambaye aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe,Mkuu wa Wilaya na Mbozi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe amesema, chanzo cha ajali kulikuwa na lori lililokuwa limeegesha njiani likibadilishwa tairi.
 
Amesema, ndipo lori lingine lililokuwa limebeba mahindi likitoka njia ya Tunduma na lingine likiwa limebeba mbao ambalo lilitokea njia ya Dar es Salaam, hawakuweza kuliona lori lilokuwa limeharibika na ndipo wakati lori lilokuwa limebeba mahindi lilipoanza kuondoka basi likatokea kwa mbele katika kulikwepa basi la Classis likaligonga lori lililokuwa limeegeshwa pembeni na kuanza kuwaka moto.
Katika ajali hiyo,RC Mgumba amesema, kati ya majeruhi 19 waliopata ajali mmoja amefariki na wengine ni majeruhi na wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Songwe na wawili hali zao sio nzuri baada ya kukatika miguu yote miwili na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Pia amesema, wamebaini kati ya majeruhi hao nane ni raia wa Tanzania na 12 ni raia wa nchi jirani ya Congo DRC. Hata hivyo, Mheshimiwa Mgumba ameahidi kutoa taarifa kamili baadae.(HabariJamiiTanzania).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news