Dakika 93 nyasi zimeumia huku Simba SC na Yanga SC wakitoka sare ya bila mabao

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WATANI wa jadi Simba SC na Yanga wameonyeshana ubabe kwa kumaliza dakika 93 kwa sare ya bila mabao.
Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya Desemba 11,2021 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,Dar es Salaam.

Awali dakika 90 zilimalizika katika dimba Benjamin Mkapa kwa wenyeji Simba kutoka suluhu ya 0-0 na Yanga, dakika tatu za nyongeza nazo hazikuongeza kitu.
Aidha,kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu huku Simba ikibadilika kiuchezaji tofauti na mwanzo mwa kipindi cha kwanza cha mchezo.

Dakika ya 63, kocha wa Simba Pablo Franco alifanya mabadiliko ya kumtoa mshambuliaji Kibu Denis na nafasi yake kuchukuliwa na Larry Bwalya ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo.
Kwa upande wa Yanga SC, Kocha Mkuu Nassredine Nabi alifanya mabadiliko dakika ya 69, ya kumtoa Jesus Moloko na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa.

Dakika ya 79, Simba iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Meddie Kagere, Bernard Morrison na nafasi zao kuchukuliwa na John Bocco na Yusuph Mhilu.
Mabadiliko ya Morrison yalizua sintofahamu dimbani baada ya kupiga mpira wa kona bila mwamuzi kuruhusu kisha kuonyesha kutokuwa tayari kutoka wakati akijiandaa kupiga mpira wa kona uliokuwa unaelekezwa upande wa Yanga SC.

Dakika ya 86, Yanga SC iliendelea kufanya mabadiliko kwenye eneo la ushambuliaji kwa kumtoa Fiston Mayele na nafasi yake kuchukuliwa na Heritier Makambo.
Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha alama 20 na kuendelea kuongoza ligi kwa alama mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya wote kucheza mechi nane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news