DC Mangwala afunga mafunzo ya Jeshi la Akiba

NA IMMA MSUMBA

MKUU wa Wilaya Ngorongoro mkoani Arusha, Raymond Mangwala amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika Tarafa ya Ngorogoro.
Akifunga mafunzo hayo Mangwala amewapongeza wakufunzi wa mafunzo na wale wote walioshiriki mafunzo hayo na hatimaye kumaliza mafunzo hayo kwani ilikuwa ni safari ndefu mpaka kuhitimu mafunzo hayo.
Mangwala amesema kuwa, ana imani kuwa mafunzo hayo yamewajengea ukakamavu, ujasiri na kujiamini kwani kwa sasa wahitimu watakuwa tofauti na wasiofanya mafunzo hayo.

“Nina imani ndugu zangu mafunzo haya yatasaidia sana kwenye ukakamvu,kwani mtakuwa ni tofauti kabisa na wasiofanya mafunzo ya mgambo kwani kwa sasa mtakuwa na hali ya kujiamini na kuwa wajasiri kutokana na mafunzo mliyopata,”amesema.

Aidha, ameongeza kuwa wahitimu hao wanatakiwa kujua ulinzi wa nchi ni wa wananchi wenyewe hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ulinzi wa nchi na kujilinda wao na familia zao.
Kwa upande wa mshauri wa mgambo wilayani Ngorongoro amesema kuwa,mafunzo hayo yalianza yakiwa na jumla ya wanafunzi 81 na ilipungua hadi kufikia 51 waliohitimu kwani wengine walishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na utoro na magonjwa mbalimbali.

“Mheshiwa mgeni rasmi wanafunzi hawa walianza wakiwa 81, lakini kutokana na sababu mbalimbali wengine waliacha kutokana na sababu kama vile utoro,afya na kushindwa kumaliza mafunzo na hivyo kufanya wanaohitimu kuwa ni wanafunzi 51,” amesema Mshauri wa Mgambo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news