Hospitali 13 za Rufaa za Mkoa zakabidhiwa ramani za vyumba vya kusafishia damu

NA MWANDISHI MAALUM

TIMU ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa (MSD) imewakabidhi wawakilishi wa Hospitali za Rufaa 13 za Mikoa nchini ramani zilizopendekezwa kwa ajili ya kukarabati na kujenga vituo vya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo.
Hatua hii imekuja baada ya MSD kuwezesha upatikanaji wa mashine na vitendanishi vya kusafisha damu kwa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Mfamasia Mkuu wa Serikali,Bw. Daudi Msasi huduma hizo zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao kwa hospitali zitakazokuwa zimekamilisha jengo na miundombinu.

Aidha, Bw. Msasi amewataka wakurugenzi wote wa hospitali hizo kutoa ushirikiano kwa MSD ili kuwezesha Serikali kupunguza gharama za huduma ya kuchuja damu nchini.

Post a Comment

0 Comments