Huu ndiyo ulikuwa muonekano wa jengo la ghorofa iliyoporomoka Dar na kuua watu wanne, kujeruhi 17

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

CHINI ni muonekano wa jengo la ghorofa kabla ya kuporomoka Desemba 6,2021 na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine 17 kujeruhiwa.

Ni baada ya jengo la ghorofa hilo lililokuwa linajengwa kuporomoka na kuangukia nyumba zilizokuwa karibu katika eneo la Goba kwa Awadhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mheshimiwa Kheri James alithibitishha kutokea kwa ajali hiyo, akisema baada ya jengo hilo lililokuwa linajengwa kuanguka limesababisha maafa kwenye nyumba zilizopo jirani, vifo na majeruhi.

Post a Comment

0 Comments