KMC FC yaichapa Geita Gold FC 2-0 mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KMC FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ni kupitia mtanange wa aina yake uliopigwa katika Desemba 5,2021 katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Abdulrazak Hamza dakika ya 47 na Matheo Anthony dakika ya 59 ndiyo waliosherehesha ushindi wa waajiri wao KMC FC.

Matokeo hayo yanaifanya KMC FC kufikisha alama tisa na kusogea nafasi ya nane.

Kwa upande wao,Geita Gold inabaki na alama zake tano katika nafasi ya 25 kwenye Ligi ya timu 26. Ni baada ya wote kucheza mechi nane hadi sasa.

Wakati huo huo wenyeji, Coastal Union wameichapa Mbeya Kwanza mabao 2-1.

Ni katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Vincent Abubakar dakika ya pili na Amani Kyata dakika ya 76 ndiyo waliowawezesha Coastal Union kung'ara huku Mbeya Kwanza limefungwa na Willy Edgar dakika ya 48.

Kwa matokeo hayo, Wagosi wa Kaya, Coastal Union inafikisha alama 11 na kupanda nafasi ya sita, wakati Mbeya Kwanza inabaki na alama saba katika nafasi ya 13 baada ya timu zote kucheza mechi nane Ligi Kuu Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments