Majangili yasalimisha nyara za Serikali nyuma ya ofisi ya kijiji,makachero wa polisi wakutana na maajabu katika doria Tanga

NA HADIJA BAGASHA

TEMBO wa Hifadhi ya Mkomazi aliyeuawa na majangili Novemba 27,2021 katika Kata ya Mkalamo Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe mkoani Tanga meno yake mawili yamesalimishwa nyuma ya ofisi ya serikali ya Kijiji cha Msasilasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema mbali na meno ya tembo pia wamekamata jino moja la mnyama aina ya kiboko vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.

Kamanda Jongo amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kituo Kikuu cha Polisi jijini Tanga.
Kamanda Jongo amesema, watuhumiwa walikutwa wakiwa wamehifadhi nyara hizo kwenye mfuko wa safleti,pia ameelezea kukamatwa kwa vipande 20 vya mnyama pori aina ya Swala vyenye uzito wa kilo 40.
Kamanda Jongo amesema, thamani ya nyara ya vipande vya Swala inafikia milioni moja na laki tano.

Kuhusu silaha zilizosalimishwa 62 kamanda Jongo amesema  silaha hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume na sheria.
Alitaja silaha hizo kuwa ni mitutu 11 ya silaha aina ya Gobore na Shortgun 6, Riffle 1 na Gobore 55.

Kuhusu watoto wa ibilisi,Kamanda Jongo ametoa rai wananchi kutosambaza taarifa za uvumi kuwa kuna mwanamke mmoja ambaye amekatwa tumbo na kutolewa mototo tumboni.

Akizungumzia kupatikana na mali za wizi Kamanda Jongo amesema, watuhumiwa nane wamekamatwa kwa kujihusisha na vitendo hivyo.
Kamanda Jongo amesema walikamata AC 10 aina ya Midea zilizoibiwa Novemba 9, 2021 kutoka kiwanda cha Cement cha Rhino pamoja na gari moja aina ya SUZUKI T534 DBW iliyotumika kubebea mali hiyo.

Mali nyingine ni tairi moja mpya ya gari Size 15 ya thamani ya shilingi 150,000,Sola Panel 1 ya Watts 30 ya shilingi 60,000, jeki moja na tani sita yenye thamani ya shilingi 60,000,pikipiki mbili aina ya TVS na Kinglion.

Kamanda Jongo pia amesema, katika Wilaya ya Lushoto walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja sugu wa vitendo vya uhalifu vya uvunjaji na kufanikiwa kukamata kuompyuta mpakato sita pamoja na kamera moja ambayo iliibiwa katika hoteli moja ya kitalii wilayai humo na watuhumiwa nane wamekamatwa.
Vifaa vingine ni vya kufanyia uvuvi haramu pamoja na samaki kilo 30 zilnazosadikiwa kuvuliwa kwa njia haramu.

Vifaa vingine vilivyookotwa kwenye boti hiyo ni Ingine HP 15 aina ya Yamaha yenye namba 6BEkel15dmh11311104, tambi30, dumu la mafuta 12HFuel line 1,viberiti 5,mipira 3 ya Oxygen ya kupumulia.
Vingine ni miwani 2 ya kuzamia na DCB 1 na watuhumiwa walifanikiwa kutoroka na kuvitelekeza vitu hivyo baada ya kuwaona askari.

Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujiepusha na vitendo vya uhalifu na badala yake wafanye shughuli zilizo halali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news