Mfuko wa Elimu wa Taifa ulianzishwa kwa Sheria Namba 8 ya mwaka 2001, ili kusaidia juhudi za Serikali katika kuwezesha maendeleo ya Elimu katika ngazi zote kwa Tanzania Bara na Elimu ya Juu kwa Tanzania Zanzibar.
Lengo la kuanzishwa Mfuko wa Elimu wa Taifa ni kuongeza nguvu za Serikali katika kugharamia miradi ya elimu, ili kuinua ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa katika mazingira ambayo hayafikiki kiurahisi.
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa nyumba nne za waalimu zilizofadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika shule ya Sekondari Kassim Majaliwa iliyopo Wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TEA Prof. Bernadeta Killian (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Ruangwa, waalimu wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa na watendaji kutoka TEA baada ya kupokea taarifa na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba nne za waalimu kwenye shule hiyo.wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) iliyofanyika wiki hii kwenye miradi hiyo, uongozi wa bodi ulionesha kuridhishwa na hatua ya utekelezaji katika miradi yote baada ya kukuta mingi ikiwa imekamilika kwa wakati na mmoja ukiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji. Kiongozi wa msafara katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TEA Prof. Bernadeta Killian aliwapongeza waalimu wa shule na viongozi wa Halmashauri zote baada ya kupokea taarifa kuhusu miradi kwenye maeneo yao na kulinganisha taarifa alizopokea na alichokiona uwandani.
Muonekano wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Msingi Mnimbila iliyopo Manispaa ya Lindi vilivyojengwa kupitia ufadhili wa miradi ya elimu chini ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TEA,Prof. Bernadeta Killian (mwenye suruali nyeusi) akiwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Lindi, waalimu wa Shule ya msingi Mnimbila na watendaji kutoka TEA baada ya kupokea taarifa na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule hiyo.
Madarasa yaliyokuwa yanatumika kwa ajili ya elimu ya awali kwenye shule ya msingi Ngwenya kabla ya mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vipya kupitia ufadhili wa miradi ya elimu chini ya TEA.
Nae mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ngwenya Bw. Masaninga Hussein Twende alibainisha kwamba, mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Ngwenya umeipandisha hadhi shule hiyo kutoka shule ya awali hadi kusajiliwa na kuwa shule ya awali na msingi ingawa bado kuna uhitaji wa darasa moja na nyumba za waalimu.Aliongeza kuwa, kabla ya ujenzi wa vyumba hivyo wanafunzi walikuwa wanaletwa kusoma hapo madarasa ya awali kama njia ya kuwaandaa kutembea kilomita zaidi ya mbili kuendelea na shule ya msingi hivyo kusababisha wengi kushindwa kutembea umbali huo na matokeo yake kuacha shule.
Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Ngwenya, mradi ambao uliipandisha hadhi shule hiyo kutoka shule ya awali na kuwa shule ya awali na msingi