Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire abaini kufanyiwa shambulio la mtandaoni

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MSEMAJI wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kusaidia kubaini wahalifu walioanzisha ukurasa katika mtandao wa kijamii wa Twitter huku wakitumia jina lake na picha yake kupotosha Watanzania.
Masau Bwire ambaye pia ni Mwalimu kitaaluma aliyebobea katika somo la Hisabati ametoa wito huo leo Desemba 8,2021 baada ya kubaini kufanyiwa hujuma hiyo.
"Hii account siyo yangu, kuna mtu/watu wameitengeneza kwa kutumia picha na jina langu kwa sababu wanazozijua wao, kunichafua, na kunigombanisha na taasisi/watu wengine ambao hawafurahii anachokiandika kama mimi nisivyokifurahia. 

"Mkiona chochote kimeandikwa kwenye account yenye picha yangu hiyo, si mimi niliyeandika, ni wapuuzi fulani waliodhamiria kunichafua kwa upuuzi wao, wapuuzeni. 

"Sijui TCRA, ni vipi wanaweza kunisaidia katika hili, polisi na vyombo vingine vya usalama...nisaidieni kukomesha upuuzi wa wapuuzi hawa ili, heshima yangu kwa jamii isiendelee kuchafuliwa na watu fulani kwa sababu wanazozijua wao. 

"Kwa nini mtu/watu wanisemee nisichokifikiria, kukiwaza kukisema, kama ni chema, kwa nini wasijipambanue kwa majina yao wanibambike mimi kwa mchongo wao! Huu ni upuuzi,"ameeleza Masau Bwire.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news