Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar, Desemba 21, 2021 kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imeeleza kuwa, Dkt. Abdalla Mohamed Juma ametuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii.

Naye Maryam Mohammed Hamid Mansab ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale na Hafsa Hassan Mbamba ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya utalii.

"Mohamed Mansour Nassor ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, kamisheni ya Utalii," imeeleza taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo imemtaja Aviwa Issa Makame kwamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara Rasimali watu, Mipango na utawala, kamisheni ya utalii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi unaanza Desemba 21,221.

Post a Comment

0 Comments