Rais Samia afanya uteuzi, mabadiliko kidogo ya wakuu wa wilaya

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu leo Desemba 4,2021 uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

Mosi amemteua Dadi Kolimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha akichukua nafasi ya Abbas Juma.

Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha Said Mtanda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwenda Wilaya ya Arusha mkoani Arusha.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amemuhamisha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abbas Juma kwenda Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments