Rais Samia ateua viongozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Mosi, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita kuanzia Januari 12, 2022.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu leo Desemba 31, 2021.
 
Pili,Mheshimiwa Rais Samia amemteua Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR). Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, Balozi Mwinyi ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre (AICC). Balozi Taji, kwa mujibu wa tarifa hiyo ni balozi mstaafu wa Tanzania nchini Ufaransa. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, teuzi hizi zimeanza rasmi Desemba 28, 2021,

Nne, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Bw.Patience Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Bw.Ntwina alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Katiba na ufuatiliaji wa Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, uteuzi huu umeanza rasmi Desemba 30,2021.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news