TAKUKURU Kiteto yamnasa Mwenyekiti kwa tuhuma za kuuza ardhi kwa watu wanane

NA MOHAMMED HAMAD

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kiteto mkoani Manyara  inamshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngeju Kata ya Namelock wilayani humo, Bw. Michael Noah Seru, kwa tuhuma za kuuza ardhi.
Mkuu wa TAKUKURU wilayani Kiteto, Venance Sangawe.

Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kiteto, Venance Sangawe amesema alifikia uamuzi wa kumkamata na kumuweka ndani Mwenyekiti huyo kwa tuhuma za kuuza ardhi na kumchunguza kisha atamfikishwa mahakamani ambapo inadaiwa alipokea fedha za watu wanane.

"Nimemkamata Mwenyekiti, Michael Noah Seru, na kumweka ndani kwanza..., tunamchungunza kwa tuhuma ya kupokea fedha za watu wanane hapa Kiteto akidai anataka kuwauzia ardhi ya kijiji jambo ambalo ni kosa kisheria, lakini pia hana ardhi na hana mamlaka ya kuuza ardhi,"amesema Sangawe.

Amesema, migogoro mingi ya ardhi Kiteto inasababishwa na baadhi ya wenyeviti wa vijiji ambao wanauza ardhi hiyo na mara kadhaa madhara makubwa yamekuwa yakijitokeza kwa wananchi yakiwemo kugombana na hata maafa kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.

Mbali na Mwenyekiti huyo alisema katika Ofisi yake kuna madai mengi yanahusu ardhi hivyo ameanza na Mwenyekiti huyo kisha ataendelea na wengine ambao wanajihusisha kuuza Ardhi katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Al Haji Batenga, katika Kikao cha Ushauri cha Wilaya ya Kiteto DCC, aliwataka wananchi kuepuka matapeli wa ardhi na kutakiwa kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya sheria.

Alisema migogoro ya ardhi Kiteto bado ipo na mingi inachangiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali za vijiji ambao wanaitumia migogoro hiyo kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.

Amesema,kamwe hatofumbia macho migogoro ya ardhi akidai sheria kali zitachukuliwa dhidi ya walanguzi wa Ardhi ambao wamekuwa na madhara makubwa kwa jamii isiyo na uelewa wa kutosha Juu ya Ardhi ardhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Hata Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kimana Yuko na tabia hiyo
    Akamatwe na afanyiwe uchnguzi

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news