Tanzania yapongezwa Kimataifa katika masuala ya utalii

NA MWANDISHI MAALUM, HISPANIA

TANZANIA imepongezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kwa namna ambavyo ilifanikisha kufanya onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini Arusha lililokuwa na lengo la kutangza utalii katika nchi za jumuiya za ukanda huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Ufaransa, Mhe.Samwel Shelukindo ( kulia) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi (kushoto) wakifuatlia Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololkashvir wakati akitaja baadhi ya nchi za Afrika ambazo licha ya changamoto ya ugonjwa wa Korona lakini zimeendelea kufanya vizuri katika suala la utalii.

Ameyasema hayo mapema jana wakati alipokuwa akitaja baadhi ya mafanikio yake katika Uongozi wake tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UNWTO katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa 24 wa UNWTO ulipoanza.

Amesema, Tanzania ni moja kati ya nchi katika bara la Afrika zinazochipukia katika kuhakikisha sekta ya utalii inafanya vizuri kwa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa ajili ya kutangaza vivutio vyake vya utalii.

Ametaja Onesho la kwanza la Utalii la Afrika Mashariki (EARTE) kuwa Tanzania imeonesha ukomavu na ujasiri wa hali ya juu katika kulifanya kwa mafanikio makubwa onesho lile licha ya kuwa na muda mfupi wa maandalizi na uwepo wa changamoto a ugonjwa UVIKO -19

''Kati ya nchi za Afrika ninazoziona zinakwenda kuongoza kimapato kwa kuifanya sekta ya utalii kuwa namba moja huwezi kuiacha kuitaja Tanzania '' am so proud of you Tanzania,'' alisema Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurabm.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( katikati ) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi ( wa kwanza kulia) wakimsiliza Mtumishi wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Hispania, Jacobr Nsihkl akilezea maeneo ya vivutio vya utalii alivyotembelea mwezi uliopita wakati alipokuja nchini Tanzania katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania.

Akizungumzia pongezi hizo, Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab kwa kuona na kukubali jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kufanya vizuri kimapato.

''Tumepongezwa kwa namna ambavyo tumeweza kufanya onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki. Sisi tuliona dogo, lakini wenzetu huku katika nyanja za kimataifa waliliona kubwa,'' alisema Dkt. Ndumbaro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa nne kulia ) akiwa Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Ufaransa, Mhe.Samwel Shelukindo ( wa kwanza kulia) akiwakabidhi zawadi mbalimbali Watendaji Wakuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO) kanda ya Afrika, Elsia Grancourt ( wa tatu kulia) pamoja na Natalia Bayona ( wa pili kushoto) katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi na kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Lily Fungamtama.

Amesema, Onesho la EARTE pamoja na mkutano huu wa UNWTO kwa nchi ya Tanzania ni fursa ya kuweza kutangaza utalii, lakini kama fursa ya kuwavuta wenzetu watalii waje pia nchini Tanzania katika kuwekeza kwenye sekta ya utalii.

Dkt.Ndumbaro amesema, pongezi hizo zinatia moyo ya kuongeza kasi zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

"Tumepongezwa na nimesema kwamba kumbe kweli watanzania wanaweza kufanya mikutano kwa kiwango kikubwa zaidi,’’ alisema Dkt. Ndumbaro.
Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill akizungumza wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kufanikisha kufanya Onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha kwa lengo la kutangaza utalii katika nchi za Jumuiya za ukanda huo.

Kupitia Pongezi hizo, Dkt.Ndumbaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan kwa Ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwake huku akitaja Kampeni maalum cha kutangaza utalii wa kupitia kipindi cha ' Royal Tour' aliyoiasisi yeye mwenyewe kuwa hali inampa nguvu zaidi katika kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro katika mkutano huo wa siku nne unaoendelea kufanyika katika Jiji la Madrid anatumia fursa hiyo ya kushiriki katika kuwaalika Viongozi mbalimbali wa Kidunia Mawaziri wa Utalii pamoja na Wataalamu mbalimbali wa utangazaji na masuala ya utalii katika kuwaalika kushiriki katika Mkuu wa Utalii wa Kanda ya Afrika ambapo Tanzania anataraji kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo utakafanyika Oktoba 6 hadi 8 mwaka 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news