TANZIA:Askofu na Mchungaji Profesa Ranwell Mwenisongole afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

CITY Christian Church (C.C.C) -TAG Upanga jijini Dar es Salaam limempoteza shujaa wa injili,Askofu Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mchungaji Kiongozi wa TAG Upanga,Profesa Ranwell Mwenisongole.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwinjilisti Dkt. Magnus Mhiche,Kaimu Katibu Mkuu na Makamu Askofu Mkuu wa TAG leo Desemba 25,2021 imethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

"Wapendwa watumishi wa Bwana kwa masikitiko makubwa Ofisi Kuu TAG Makao Makuu Dodoma inawataarifu msiba uliotupata wa kuondokewa na shujaa wetu Askofu Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mchungaji Kiongozi wa TAG Upanga Rev Dr Ranwell Mwenisongole.

"Shujaa amerudi nyumbani.Mungu aifariji familia na kanisa kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Taarifa zingine zaidi mtajulishwa baadae.Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe,"ameeleza.

Post a Comment

0 Comments