Tuwasaidie wajasiriamali wadogo mikopo yenye riba nafuu-RC Kagaigai

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imetaka asasi za kifedha kusaidia wajasiriamali wadogo kupata mikopo yenye riba nafuu badala ya kuwaacha waangukie katika mikopo umiza inayoua mitaji yao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa huo, Steven Kagaigai wakati anazungumza na watumishi wa Uchumi Commercial Bank (UCB) wilayani Siha kwenye maonesho ya bidhaa katika miaka 60 ya Uhuru iliyofanyika viwanja vya CCM wilayani Siha.
RC huyo ametaka UCB pamoja na asasi nyingine kutengeneza mifumo rafiki kwa wajasiriamali na wakulima wadogo ili kukuza mitaji yao badala ya kuwaacha wafilisike.
Msimamizi wa tawi la UCB Ltd, James Kileo akifafanua jambo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai wakati wa maonesho ya bidhaa mbalimbali kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru yaliyofanyika kimkoa wilaya ya Siha.

Kagaigai amesema kwa miaka 60 ya Uhuru, Taifa limepiga hatua kubwa za maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo, Nishati na miundombinu ya barabara hivyo ni wajibu wa wadau wa maendeleo wakaunga mkono juhudi za serikali.

Awali Kileo amesema, benki inatoa huduma za aina mbalimbali na tayari imewezesha wajasiriamali zaidi ya 1,000 mkoani hapa ambao baadhi wamefungua viwanda vidogo na kuajiri watu wengine.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Siha, Thomas Apson amewataka wananchi na wajasiriamali kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya wilaya, lakini waombe fedha nyingi na si kidogo kama wanavyofanya mara kwa mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news