Yanga SC yasema Simba lazima wakae, Sogne kuikosa Kariakoo Derby

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

YACOUBA Sogne ambaye ni mshambuliaji wa Wanajwangwani, Yanga SC atakuwa mchezaji pekee kwa upande wa klabu hiyo atakayekosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Desemba 11, 2021 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa klabu hiyo,Hassan Bumbuli ambapo mtanange huo wa watani wa jadi maarufu kama Derby ya Kariakoo tambo zimeanza kila kona.

“Tumejiandaa kushinda mchezo huo, mpaka sasa kikosi chetu kipo vizuri na hadi nakuja hapa taarifa nilizozipata kutoka kambini wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokuwa Yacoub Sogne, ambaye ni majeruhi.

“Dhamira yetu ni kupata matokeo ambayo yatatuongezea nafasi ya kulisogelea Taji la Ligi Kuu ambalo tumelikosa kwa muda mrefu, tunaamini msimu huu taji hili lina kila sababu ya kurudi nyumbani,” amesema Bumbuli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news