Bodi yaufungia Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani tena

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BODI ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imeufungia tena Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani baada ya kubaini bado haukidhi vigezo vya mechi za Ligi Kuu ya NBC.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TPLB imeeleza kuwa, eneo la kuchezea la uwanja huo linatakiwa kusawazishwa vizuri na majani yake kustawishwa vema ili uweze kuendana na matakwa ya kikanuni na sheria namba moja ya mpira wa miguu inayozungumzia uwanja.

Aidha,kufuatia taarifa hiyo, klabu ya Ruvu Shooting ambayo ilikuwa ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani italazimika kuhamia uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.

Kamati ya leseni za klabu itaukagua uwanja huo mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ili kujiridhisha kuwa unafaa kuendelea kutumika kwa michezo ya ligi.

Aidha,bodi inaendelea kuzikumbusha klabu zote kuhakikisha viwanja vyao vya nyumbani vinakuwa katika hali nzuri wakati wote kwani viwanja ambavyo vitakosa sifa vitafungiwa mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news