Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar atoa shukurani MAALUM kwa wote walioshiriki katika mazishi na maziko ya kaka yake Mwalimu Said Masoud Othman

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, pamoja na Familia yake, wanatoa shukurani za dhati kwa wananchi wote, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Pemba, Viongozi Wakuu wa siasa kutoka vyama mbalimbali, na zaidi wananchi wa Kijiji cha Pandani na vitongoji vyake, walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika msiba wa mpendwa wao marehemu Mwalimu Said Masoud Othman.
Mwalimu Said ambaye ni kaka wa Makamu wa Kwanza wa Rais, alifariki dunia usiku wa kumkia Jumamosi ya tarehe 15 Januari 2022 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kisiwani Unguja, na kuzikwa siku hiyo hiyo ya Jumamosi majira ya Alasiri huko Kijijini kwao Masipa Pandani Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Hayo yamebainishwa leo Januari 18,2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Aidha, shukurani maalum na za kipekee ziwaendee Viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo kutoka ngazi za Tawi hadi Taifa kutokana na kuonesha moyo wa upendo na ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha msiba wa mpendwa wao huyo.

Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news