Makamu wa Rais Dkt.Mpango afiwa na kaka yake

NA MWANDISHI MAALUM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amefiwa na kaka yake Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Gerald Mpango. Askofu Gerald Mpango amefariki tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa nyumbani kwa marehemu Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango ambaye ni kaka yake aliyefariki Jana tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam. Januari 20,2022.

Enzi za uhai wake Askofu Gerald Mpango alihudumu katika kanisa la Anglikana Dayosisi ya Magharibi ya Tanganyika ( Diocese of Western Tanganyika) 

Mazishi ya Askofu Mstaafu Gerald Mpango yanatarijiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 wilayani Kasulu Mkoani Kigoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali waliofika nyumbani kwa marehemu Askofu Mstaafu Gerald Mpango Boko Jijini Dar es salaam. Marehemu Askofu Mstaafu Gerald Mpango ni kaka wa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. Januari 20,2022.

Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa tarehe 21 Januari 2022. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na marehemu kaka yake Askofu Mstaafu Gerald Mpango tarehe 16 Desemba 2021 wakati Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoani Kigoma. Askofu Mstaafu Gerald Mpango alifariki jana tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam. (PICHA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

Baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kisha kufuatiwa na Ibada ya kuaga mwili huo katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu Kigoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news