TAKUKURU Dodoma yabuni tiba mapambano dhidi ya rushwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma imeanza kutekeleza mkakati wa kuwaelimisha vijana ambao ni wanachama wa Skauti na waliopo kwenye klabu za wapinga rushwa kuhusu nafasi zao ili kuzuia vitendo vya rushwa katika jamii wanamoishi.

Skauti ni chama cha hiyari cha kielimu kinachotoa mafunzo kwa vijana wote bila ubaguzi wa rangi,jinsia,dini wala kabila ambapo TAKUKURU inatumia nafasi hiyo ili kuhamasisha ushiriki wa jamii katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthens Kibwengo

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthens Kibwengo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema, lengo ni kuwa na watumishi wa sekta za umma na binafsi na wananchi kwa ujumla ambao ni wazalendo na ambao wanaichukia rushwa kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Kibwengo amesema, katika eneo la uelimishaji umma ili kuhamasisha ushiriki wa jamii kwa ujumla katika mapambano dhidi ya rushwa, wamefanya mikutano 47 ya hadhara, semina 90, onesho moja kwa lengo la kuimarisha klabu 121 za wapinga rushwa zilizopo kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo. 

"Tulishiriki katika vipindi 12 vya redio, baadhi ya mikutano ya hadhara ilifanyika kwa utaratibu wa 'TAKUKURU INAYOTEMBEA' ambapo kwa kutumia gari la matangazo tuliwahamasisha wafanyabiashara kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa biashara, kutambua umuhimu na wajibu wa kulipa kodi, kutotoa wala kushawishi kutoa rushwa,’’amesema.

Pia amesema kuwa,kwa kushirikiana na wadau wengine waliweka nguvu nyingi kufuatilia madarasa yaliyojengwa kwa fedha na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19 pamoja na madarasa jumla ya miradi 596 ilikaguliwa.

‘’Ushauri ulitolewa kwa wahusika kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto. Kati ya miradi hiyo minne, miradi mitatu kati yake ilikutwa na dosari ndogo ndogo, ambazo zilijadiliwa na kurekebishwa, lakini kwenye mradi mmoja inaonekana malipo yaliyofanyika bila kazi husika kutekelewa, hivyo tunashirikiana na halmashauri husika kufuatilia marekebisho ya dorasi hiyo,’’amesema.

Mkuu huyo amesema, katika kuzuia vitendo vya rushwa walifanya chambuzi za mifumo tisa ya utendaji na utoaji huduma katika mkoa wa Dodoma na kushirki warsha 11 za kujadili matokeo ya uchambuzi wa mifumo hiyo mkoani hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news