Mheshimiwa Masanja azindua Mtandao wa Wanawake Lakimoja Dar es Salaam

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amezindua Mtandao wa Wanawake Laki moja jijini Dar es Salaam unaohusika na kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na kukwamua wanawake kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Masanja amewataka wanawake kushiriki kupinga ukatili wa kijinsia na pia kushirikiana katika kujenga uchumi wa Taifa. 

Kuhusu Sekta ya Utalii, Mhe. Masanja amewahamasisha wanawake kuwekeza katika Sekta hiyo ili kuinua vipato vyao akitolea mfano uwekezaji kwenye huduma za malazi, chakula, usafiri na nyingine nyingi.
Aidha, Mhe. Masanja ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza vyema Taifa na kuwaheshimisha watanzania na pia kuwa Mwanamke wa kuigwa kwa kuongoza njia kwa wanawake.

Post a Comment

0 Comments