Muonekano mpya wa Baraza la Mawaziri chini ya wizara 22

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 8,2022 amefanya mabadiliko ya muundo wa wizara, uteuzi wa mawaziri na manaibu mawairi na kuwahamisha wizara mawaziri na naibu mawaziri.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein A.Kattanga huku akisisitiza kuwa, uteuzi huo wa mawaziri na naibu mawaziri umeanza leo Januari 8, 2022 na uapisho utafanyika Januari 10, 2022 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Katika uteuzi na mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na wizara zenye muundo mpya ikiwemo ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Wizara nyingine ni Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikiwemo Wizara ya Afya.

Mawaziri wapya

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa ni; mawaziri watano ambao ni Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Mheshimiwa Hamad Y.Masauni aliyekuwa Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Dkt.Pindi H.Chana kuwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Nne, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Dkt.Angelina S.Mabula aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tano, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Mheshimiwa Hussein M. Bashe aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuwa Waziri wa Kilimo.

Manaibu Waziri wapya

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia ameteua manaibu waziri watano, mosi amemteua Mheshimiwa Anthony P.Mavunde kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo. Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mheshimiwa Jumanne A. Sagini kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua,Dkt.Lemomo Ole Kiruswa kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Madini, nne Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tano, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Mheshimiwa Atupele Fredy Mwakibete kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi).

Mawaziri waliohamishwa

Katika hatua nyingine,Mheshimiwa Rais Samia amewahamishia wizara nyingine mawaziri na manaibu waziri mbalimbali.

Mawaziri tisa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mabadiliko hayo amewahamishia katika wizara nyingine mawaziri tisa.

Mosi, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J.Mhagama kwenda kuwa Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwenda Wizara ya Afya.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Gorge B.Simbachawene kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Nne, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha Profesa Joyce L.Ndalichako kutoka Wizara ya Elimu kwenda kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Tano, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent L. Bashungwa kwenda Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Sita, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf F. Mkenda kwenda Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Saba, Mheshimiwa Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Mheshimiwa Dkt. Dorothy O.Gwajima kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum.

Nane, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed O.Mchengerwa kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Tisa, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (TEHAMA), Mheshimiwa Dkt.Ashatu K.Kijaji kwenda Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Manaibu mawaziri watatu

Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Khamis H.Khamis kwenda Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Pili, Mheshimiwa Rais amemuhamisha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Hamad H. Chande kwenda Wizara ya Fedha na Mipango.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemuhamisha aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Mwanaidi A. Khamis kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

ORODHA YA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI KATIKA WIZARA 22 KUFUATIA MABADILIKO YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA NI KAMA IFUATAVYO;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news