Mwalimu Makuru afunguka kuhusu mawaziri, makatibu wakuu

NA FRESHA KINASA

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini, Mwalimu Makuru Lameck Joseph amesema mawaziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan wanawajibu wa kufanya kazi kwa kuzingatia shabaha ya teuzi zao katika kukidhi malengo ya Rais aliyewaamini kuwateua wamsaidie kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa Watanzania. 
Mwalimu Makuru amesema, hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaamini na kuwateua ameona kuwa wana uwezo mzuri wa kumsaidia kutatua kero mbalimbali za wananchi na kushiriki kikamilifu katika ajenda ya kuliletea maendeleo Taifa. Hivyo watumie vyema nafasi zao kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, upendo, juhudi na kwa moyo thabiti. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na DIRAMAKINI BLOG Mjini Musoma ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza kwa kuteuliwa kwao na kusema kuwa kila mtanzania anapaswa kuwaombea na kuwapa ushirikiano wa dhati katika safari yao ya kuwatumikia wananchi. 
Amesema, hawapaswi kujisahau na kulewa madaraka kwani teuzi ambazo zilifanyika nyuma baadhi ya viongozi walioteuliwa walilewa sifa na kushindwa kuwajibika kikamilifu na kwa uaminifu pasipo kuelewa kuwa wao wapo madarakani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si vinginenvyo

Ameongeza kuwa,Taifa lina hazina kubwa ya viongozi ambao hawajapata nafasi ya kuteuliwa, lakini wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo. 

Hivyo viongozi walioteuliwa wamshukuru Rais Samia na kudra za Mwenyezi Mungu kwa kuwapa kibali cha kuwatumikia watanzania wasijisahau hata kidogo kwa kutowajibika kikamilifu kutatua matatizo nankero za wananchi hatua ambayo inaweza ikamvunja Rais moyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na mawaziri na manaibu mawaziri katika kikao kazi kilichofanyika Januari 13, 2022 katika Ukumbi wa HAZINA jijini Dodoma. (Picha na Ikulu).
 
"Wanawajibu wa kuwajibika kufanya kazi kwa weledi na kwa kufuata sheria za nchi pasipo kuwakandamiza na kuwaonea wananchi. Wajikite katika ajenda za kuleta maendeleo kwa wananchi wakimsaidia Rais pasipo kupendelea, kubagua mtu yeyote ama kumuomea mtu bali watende haki kama sheria na miongozo ya nchi inavyotaka na kwa kuzingatia viapo vyao walivyoaapa baada ya kuapishwa,"amesema Mwalimu Makuru.
 
Pia, amewaasa waache makundi, majungu, fitina, unafiki na kujipendekeza kwani hayo yote ni adui wa haki na ni vikwazo vya maendeleo katika Taifa ambavyo hatimaye huleta sintofahamu kwa wananchi na migawanyiko ambayo nadni yake huleta chuki miongoni mwa wananchi na viongozi wanaowaongoza. 
"Cheo ni dhamana ama koti la kuazima.Viongozi wote wawajibike kufanya kazi vyema wakitambua wasipofanya kazi kwa weledi na kuendana na kasi ya Rais wetu mpendwa watavuliwa madaraka hayo. Hivyo wasimame kidete kuwatumikia wananchi na kuwatetea wananchi katika kuwaletea maendeleo Kama ambayo ilani ya Chama Cha Mapinduzi yenye kurasa zaidi ya 300 inavyosema,"amesema Mwalimu Makuru. 

Katika hatua nyingine, Mwalimu Makuru amewaomba Watanzania wote waendelee kumuamini Rais Samia Suluhu Hassan kwani shabaha yake iko wazi kwa Watanzania kuwafikisha mahali pazuri sana kimaendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Binafsi nawaombea sana lkn pia nakuombea wewe upate mpenyo kwani nayakubali mawazo yako na ninaona uelekeo mzuri kwako. Mungu akubariki na akutangulie.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news