Ninaposema sijaja kutengua torati nina maana ya kuwa nimekuja kuongeza nguvu kiutendaji ili kumsaidia Mheshimiwa Rais kuboresha Utumishi wa Umma-Waziri Mhagama

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema amedhamiria kuimarisha misingi ya utendaji kazi kwenye Utumishi wa Umma ili wananchi wanufaike na huduma zitolewazo na taasisi za umma nchini.

Mhe. Jenista amesisitiza kuwa, ujio wake katika ofisi hiyo, sio wa kutengua torati, bali ni kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha Utumishi wa Umma.

“Ninaposema sijaja kutengua torati nina maana ya kuwa nimekuja kuongeza nguvu kiutendaji ili kumsaidia Mhe. Rais kuboresha Utumishi wa Umma na kuendeleza mazuri yaliyokwishafanyika na watangulizi wangu,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments