Orodha ya majina zaidi ya 1,000 ya vijana walioitwa kwenye usaili nafasi ya ajira kwa Cheo cha Konstebo wa Uhamiaji

NA GODFREY NNKO

IDARA ya Uhamiaji nchini imetoa orodha ya majina zaidi ya 1,000 ya vijana walioomba nafasi ya ajira kwa Cheo cha Konstebo wa Uhamiaji kupitia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa ajili ya usaili.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 28, 2022 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji,SI Paul Msele.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waombaji ambao wapo katika orodha hapa chini wanapaswa kufika kwenye usaili utakaofanyika katika Ukumbi wa Auditorium uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) siku ya Jumapili ya Februari 6, 2022 saa mbili kamili asubuhi.

"Kwa wale waliotuma maombi yao kupitia Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar wanatakiwa kufika makao makuu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) siku ya Jumapili ya Februari 6, 2022 saa mbili asubuhi,"ameeleza.

Msemaji Mkuu huyo amefafanua kuwa, waombaji wote wanatakiwa kufika na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), vyeti halisi vya taaluma, cheti cha kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kutoka JKT/JKU, kalamu ya wino ya buluu, vyeti vingine vya uhitimu wa mafunzo katika fani mbalimbali.

"Kwa waombaji ambao muundo wa fani zao unatakiwa kusajiliwa na Bodi za Taaluma wanatakiwa kufika na vyeti halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi kwa fani husika. Aidha, wasailiwa wote wanatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi husika,"ameongeza;

Post a Comment

0 Comments