Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi wa taasisi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi. 

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Januari 27,2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa uteuzi huo ambao umeanza Januari 27, 2022, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Said Seif Mzee kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Rahma Salim Mahfoudh kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua, Akif Ali Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua CDR Mohamed Khamis Makame kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Meli Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news