Orodha ya watumishi 1,544 waliopata vibali vya uhamisho kwa kubadilishana vituo vya kazi kuanzia Novemba, 2021 hadi Januari,2022 kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI

NA GODFREY NNKO

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa watumishi 1544 wa kubadilishana vituo vya kazi kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.

Profesa Shemdoe amesema kuwa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inaendelea kufanyia kazi uhamisho wa kubadilishana tu kwa sasa na kwa wale walioomba uhamisho usiokuwa wa kubadilishana kuanzia Jualai 2022 hadi Januari,2022 kwenda halmashauri za wilaya waendelee kusubiri wakati tathimini kwenye halmashauri zote ikiendelea kufanyika ili kufanya msawazo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 30, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Ofisi ya Rais TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pia Katibu Mkuu amewatraka watumishi wa mamlaka za Serikali za mitaa waliowasilisha maombi yao ya uhamisho OR-TAMISEMI kwa kipindi cha Januari 2018 hadi Juni, 2021 kuomba upya kuhamia kwenye maeneo hayo ila isiwe kwenye majiji, manispaa na halmashauri za miji.

Amesema, maombi hayo ya uhamisho yazingatie taratibu zote za uhamisho kama ilivyoainishwa kwenye Waraka wa Uhamisho Na.2 wa mwaka 2018.

Pia amewataka watumishi waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye halmashauri zao na si kwenda Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo na kuwa orodha ya majina ya watumishi waliopata vibali vya uhamisho inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Amesema, endapo mtumishi atakuwa na changamoto yeyote asisite kupiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja namba za simu +255735-160210, +255262-260210 au kuandika barua pepe kwenye anwani ya huduma@tamisemi.go.tz

Wafuatao hapa chini ndiyo watumishi waliopata vibali vya uhamisho kwa kubadilishana vituo;
Kwa majina zaidi endelea katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

Post a Comment

0 Comments