NAIBU WAZIRI SAGINI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UMWAGILIAJI, UJENZI WA GHALA GEREZA LA IDETE MOROGORO

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameweka mawe ya Msingi katika Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji na Ujenzi wa Ghala la Kuhifadhi Mazao, gereza la Idete lililopo Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akikagua Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji wa Gereza la Idete lililopo Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Januari 29,2022.

Akilipongeza Jeshi la Magereza kwa ujasiriamali na kazi nzuri wanayoifanya amelitaka jeshi hilo kuhakikisha mradi unakuwa na matokeo yanayolingana na thamani ya fedha zilizotumika pamoja na kukidhi vigezo vyote vya kitaalam pale utakapo kamilika.

“Hakikisheni mradi unakuwa na matokeo yanayolingana na thamani ya fedha zilizo tumika na kilimo mnacho kifanya kinakidhi vigezo vyote vya kitaalam ilikiwe na tija stahiki,”amesema.

Naibu Waziri Sagini amesema hayo Januari 29, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilombero, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hanji Godigodi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee, wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilombero na Maafisa mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalma mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Ghala la Kuhifadhia na Kuongezea thamani mazao katika Gereza la Idete lililopo Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro.  

Pia amelitaka Jeshi la Magereza kuendelea kubaini maeneo mengine yanayoweza kuendelezwa katika matumizi ya rasilimali ili kuzalisha mazao mengine kwa njia ya umwagiliaji bila kusubiri mvua.

“Nalipongeza Jeshi la Magereza kwa kuiona fursa na kutumia Rasilimali Maji kuzalisha Mpunga kwa wingi ambao utalisaidia Jeshi kutekeleza agizo la Serikali la kujitosheleza kwa chakula. Andaeni maandiko ya miradi yanayoweza kuishawishi Serikali ili iweze kutenga Fedha kwa ajili ya kugharamia miradi hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini ( Wapili Kulia) akionyeshwa mchoro wa ramani ya Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Ghala la Kuhifadhia na Kuongezea thamani mazao katika Gereza la Idete lililopo Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro.

Aidha, Naibu Waziri Sagini amelitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha wanajenga uhusiano mwema na jirani hususani wananchi wanaojishughulisha na kilimo kwa kuwawezesha kupata mgao wa maji kwa ajili ya shughuli zao za kilimo na utaalam unaoweza kuwasaidia kuongeza tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news