Shule binafsi zaiachia Serikali nafasi moja katika 10 bora Kitaifa, wasichana wawaonea huruma wavulana kwa kuwaachia nafasi mbili, wao wakomba nafasi zote 10 bora Kitaifa Matokeo Kidato cha Nne

NA GODFREY NNKO

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema jumla ya watahiniwa 483,820 sawa na asilimia 87.30 wamefaulu Mitihani wa Kidato cha Nne 2021.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amesema hayo leo Januari 15, 2022 wakati akitangaza matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na nne jijini Dar es Salaam. Tazama matokeo yote hapa>>>

Dkt.Msonde amesema, kati ya watahiniwa 483,820 wasichana waliofaulu 218,174 sawa na asilimia 85.77 huku wavulana wakiwa 204,214 sawa na asilimia 89.00 wamefaulu.

“Mwaka 2020 watahiniwa 373,958 sawa na asilimia 85.84 wa shule walifaulu mtihani huu. Hivyo ufaulu wa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa asilimia1.46 ikilinganishwa na mwaka 2020,” amesema Dkt. Msonde.

Pia katika matokeo hayo, Dkt. Msonde amesema shule ya Kemebos ya Kagera imeshika nafasi ya kwanza katika 10 bora kitaifa ikifuatiwa na shule za St. Francis (Mbeya), Waja (Geita), Bright Future Girls (Dar es Salaam) Bethel Sabs Girls (Iringa), Mau Seminary (Kilimanjaro) na Feza Boys’ (Dar es Salaam).

Shule nyingine ni Precious Blood ya mkoa wa Pwani, Feza Girls’ (Dar es Salaam) na Mzumbe ya mkoani Morogoro.

Aidha,Msonde amesema,Consolata Lubuva aliyekuwa akisoma St Francis ameibuka wa kwanza kitaifa katika orodha ya 10 bora ya watahiniwa waliofanya vizuri.

Kwa kina

Aidha,kwa mujibu wa NECTA wanafunzi wote 10 bora wanatoka katika shule zinazomilikiwa na watu binafsi isipokuwa Ilboru.

Katika 10 bora ni wavulana wawili tu ndiyo wamepenya huku nafasi zote zikibebwa na wasichana.

Aidha,nafasi tano za juu zimechukuliwa na wanafunzi wasichana kutoka Shule ya St. Francis Girls ya mkoani Mbeya ambapo Consolata Prosper Lubuva wa shule hiyo ndiye aliyetajwa kuwa mwanafunzi bora kitaifa.

Pia nafasi ya pili imeenda kwa Bhutoi Ernest Nkaganza huku Wilihelmina Steven Mijarifu akishika nafasi ya tatu, Glory John Mbele akishika nafasi ya nne na Mary George Ngoso akifunga tano bora ambayo wanafunzi wote wametoka St.Francis ya jijini Mbeya.

Naye Holly Beda Lyimo kutoka Shule ya Sekondari Bright Future Girls ya jijini Dar es Salaam ameshika nafsi ya sita huku Blandina Karen Chiwawa (St Francis) amechukua nafasi ya saba.

Imam Suleiman Mogaeka kutoka Feza Boys ya jijini Dar es Salaam nafasi ya nane, nafasi ya tisa ni Hamisi Madili wa Shule ya Sekondari ya Ilboru ya mkoani Arusha inayomilikiwa na Serikali huku Clara Straton Assenga wa St. Francis akichukua nafasi ya 10 bora Kitaifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news