Simba SC yakosekana katika tano bora ya vinara wa mabao, Yanga SC yapiga kote kote

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzania (TFF) limetoa orodha ya vinara wa mabao Ligi Kuu ya NBC 2021/2022 hadi kukamilika kwa mzunguko wa 11.

Kwa mujibu wa TFF, vinara walioingia tano bora kwa kufunga mabao mfanano kwa maana ya matano kila mmoja ni Reliants Lusajo wa Namungo FC, George Mpole wa Yanga SC, Jeremia Juma wa Tanzania Prisons na Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania FC.
Wakati huo huo, TFF imewataja waliopachika mabao manne kila mmoja kuwa ni Meddie Kagere wa Simba SC, Richardson Ng'ondya wa Mbeya City FC, Feisal Salum Toto wa Yanga SC na Juma Luizio wa Mbeya City FC.

Post a Comment

0 Comments