Simba SC,Yanga SC watumia mbinu mfanano kutembeza kichapo Kombe la Mapinduzi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBINU wanazotumia Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi unaweza kukiri wazi ndizo hizo hizo wanazotumia Yanga SC kuhakikisha wanatwaa taji hilo.

Ushindi wa leo ambao ni mfanano wa magoli mawili unaashiria kuwa, watani hao wa jadi wana jambo moja ambalo ni kila mmoja kuhakikisha anaondoka na kikombe hicho.
Awali Simba SC wameanza vyema michuano hiyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Selem View katika mchezo wa Kundi C uliopigwa dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Pape Ousmane Sakho dakika ya 25 na kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 53 ndiyo waliowanyanyua mashabiki wa klabu hiyo.
Aidha,kabla ya chereko chereko za Wanasimba hazijaisha, watani wao Yanga SC wamekoleza moto.

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo wameacha kilio kwa Taifa Jang'ombe kwa kuwabamiza mabao mawili kwa sufuri.

Dakika ya 32,Ebenezer Makambo aliwanyanyua mashabiki wa Yanga huku Dennis Nkane dakika ya 50 akiwaliza kabisa Taifa Jang'ombe.

Katika mechi za kwanza,bao pekee la mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda liliwapa Azam FC alama tatu.

Azam FC walitembeza kichapo hicho kwa Meli 5 City katika mchezo wa Kundi A uliopigwa Jumanne hii dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Nao Namungo FC ilishinda pia 2-0 dhidi ya wenyeji wengine, Yosso Boys, Kundi A pia hapo hapo Uwanja wa Amaan.

Mabao ya Namungo FC yalifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90.

Post a Comment

0 Comments