Yanga SC yaanza kusukwa upya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga yenye maskani yake jijini Dar es Salaam imeendelea na maboresho ya kisasa kwa ajili ya kuifanya klabu hiyo kongwe kuwa na ushindani mkubwa Kitaifa na Kimataifa.
Maboresho hayo yanalenga katika nyanja mbalimbali ya klabu ikiwemo aina ya mfumo wa uendeshaji huku ikijikita zaidi kujiendesha kidijitali.

Katika jitihada hizo za maboresho, leo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, Mtendaji Mkuu wa klabu, Senzo Mazingiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh na Mkuu wa bidhaa ya N-Card, Khalifa Mwinyi wamesaini mkataba wa makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali.
Ni kadi zitakazotumiwa na wanachama, ikiwa ni sehemu ya hatua za awali za mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo. 

Kwa mujibu wa taarifa za awali, kadi moja itauzwa kwa sh.29,000 kwa wanachama.

Yanga wameipa Kilinet jukumu la kusimamia na kuendesha mfumo wa kidigitali (Digital Platforms za Yanga), usajili wa wanachama na mitandao ya kijamii ya klabu.
Kwa upande wa N-Card watakuwa na jukumu la kutengeneza kadi za uanachama ambazo zitawawezesha wanachama kuzinunua katika mfumo wa kielektroniki.

Wakati huo huo, Yanga imemtambulisha mshambuliaji Crispin Ngushi kutoka Mbeya Kwanza kuwa mchezaji wake mpya wa nne katika dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa wiki ijayo.
Ngushi anaungana na wachezaji wengine watatu, kipa Abdultwalib Mshery kutoka Mtibwa Sugar na viungo Dennis Nkane kutoka Biashara United na Salum Abubakar kutoka Azam FC kufanya idadi ya wachezaji wanne wapya hadi sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news