TANZIA: Mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Mbeya Press Club, Festo Sikagonamo afariki


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

ALIYEWAHI kuwa Mwandishi wa Habari wa Redio One na ITV kutoka Mbeya, FESTO SIKAGONAMO amefariki.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizoifikia DIRAMAKINI BLOG amefariki akiwa ni Mwenyekiti wa Mbeya Press Club.

SIKAGONAMO aliwahi kutwaa tuzo mbalimbali kutokana na ubunifu na kazi nzuri kabla ya kuondoka IPP kwenda kutafuta maisha maeneo mengine.

Wakati huo huo,Kamati Tendaji ya Mwanza Press Club leo Januari 7,2022 imetoa salamu za pole kwa klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mbeya kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake huyo.

"Klabu ya Waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza imepokea kwa masikitiko kifo cha Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mbeya, Bwana Festo Sikagonamo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Januari, 7, 2022 Jijini Mbeya.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Katibu wa Mbeya Press Club Bwana Keneth Mwakandyali kwa simu alipoongea na Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Bwana Edwin Soko.

Kamati tendaji ya MPC, wanachama na MPC na waandishi wote wa Mkoa wa Mwanza wanatoa pole kwa Mbeya Press Club, Ndugu Jamaa na wanafamilia wa marehemu Festo Sikagonamo Mwakasege kwa msiba huo mzito.

MPC inatambua mchango uliotukuka wa marehemu tangia alipokuwa akifanya kazi kwenye vyombo vya habari mbalimbali vya habari ikiwemo TBC na hadi kwenye nyanja ya uongozi alipokuwa Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimisha.

Marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake kiweledi na mwenye msimamo kwenye tasnia ya habari Tanzania.

Tuna amini sisi tulimpenda lakini wenyezi Mungu alimpenda zaidi jina lake lihidimiwe,"imefafanua taarifa hiyo.

Kazi ya Mungu haina makosa. Mwenyenzi Mungu amlaze mahali pema. Amen

DIRAMAKINI BLOG inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news