TRC yathibitisha ajali ya treni iliyouwa mtoto,kujeruhi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa treni ya abiria yenye injini namba 9022 imepata ajali majira ya saa 10 alfajiri ya leo Januari 16,2022  kati ya Mkalamo na Mvave Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.

Treni hiyo ilikuwa inatokea Arusha kuelekea Dar es salaam ikiwa na mabehewa 14 yenye abiria 700 ambapo mabehewa 5 yalipinduka na mengine manne yaliacha njia na kupelekea majeruhi watano na kifo cha mtoto mmoja mwenye umri wa miaka saba.
TRC imesema wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu kufahamu chanzo cha ajali hiyo ili kuchukua hatua zaidi;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news