UVCCM wafika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kuwajulia hali wagonjwa, kufanya usafi

NA DOREEN ALOYCE

KATIKA kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Chaha Mapinduzi (CCM),Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM Wilaya ya Dodoma wametembelea Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa,kupanda miti pamoja na kufanya usafi.
Akizungumza kwenye zoezi hilo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Dodoma, Said Kasote amesema kuwa katika kuafhimisha miaka 45, ya kuzaliwa chama hicho wameona kutumia fursa hiyo kufanya kazi za kijamii ambazo zitaweka alama kwa Taifa.

Kasote amesema kuwa, waliamua kwenda kwenye hospital hiyo ya Mirembe kwani ni eneo la kimkakati ambalo limesahaulika na jamii ambapo inaonekana kama hosptiali ya wilaya jambo ambalo sio sahihi.

"Chama Cha Mapinduzi CCM ni chama cha kijamii, tunaamini katika ujamaa na kujitegemea,  hivyo tumefanya tukio ili kwa ajili ya k utoa motisha kwa jamii hususani kupanda miti,kufanya usafi kutembelea wagonjwa jambo ambalo linatia moyo na ishara ya upendo katika maisha yetu," amesema Kasote.
Pia amesema katika kuadhimisha kuzaliwa kwa chama hicho, Umoja wa Vijana Wilaya ya Dodoma wako mstari wa mbele na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,Rais Samia Suluhu Hassan kumpigania ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Jaskon Mjinja ni Katibu wa Afya Hospital hiyo ya Mirembe amesema, umoja huo wa vijana wamefanya kitendo cha kihistoria kutoa huduma kwa wagonjwa kwani hivi sasa wamesahaulika kwa jamii ukizingatia afya ya akili ni jambo kubwa sana Kitaifa.

Amesema, jamii imekuwa ikichukulia vibaya hospital hiyo kuwa imejikita kwa wagonjwa wenye afya ya akili jambo ambalo sio kweli bali huduma zote zinatolewa na kuna wataalamu wengi na kuwataka wananchi wenye uhitaji wa kushauriwa kisaikolijia kufika kwa ajili ya matibabu.
"Licha ya hayo tuna changamoto hususani za mazingira,lakini tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya fedha za UVIKO-19 ambapo tumejenga jengo la emergency department na ICU ambavyo votakamilika mwezi wa pili mwaka huu,"amesema Mjinja.

Akitoa maelezo juu ya huduma wanazozitoa kwa wagonjwa wa afya ya akili katika hospitali hiyo, Mtaalamu wa Tiba Kazi kiongozi, Julia Dagwa amesema kuwa wanawafundisha kazi ndogo ndogo za kujihudumia ikiwemo kupiga mswaki,kuoga na kufua sambamba na shughuli za burudani.
"Lakini pia tuna shughuli za uzalishaji ambapo tunalima matunda,mboga za majani lengo ni kuutafsiri ubongo kumtambua mmoja mmoja na kumrekebisha na baada ya hapo tunaangalia kama kuna uwezekano wa kumruhusu kwenda nyumbani na kupitia elimu hiyo inawasaidia kuishi vizuri na jamii inayowazunguka,"amesema Julia.

Kwa upande wao Vijana wa Umoja huo wamesema kupitia tukio hilo wamejifunza mambo mbalimbali ya uzalendo na kushirikiana na shughuli za kijamii. 

Hata hivyo, kilele cha sherehe hizo za kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM zinatarajiwa kufanyika rasmi tarehe 5 Februari, mwaka huu mkoani Mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news