Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 7, 2022

NA GODFREY NNKO

RANDI ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 145.09 na kuuzwa kwa shilingi 146.47 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.22 na kuuzwa kwa shilingi 20.39.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 7, 2022 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.28 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.14.

Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3094.93 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3126.81.

Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2586.92 na kuuzwa kwa shilingi 2613.02.

Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 358.62 huku ikiuzwa kwa shilingi 361.75 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.74 na kuuzwa kwa shilingi 19.93.

Post a Comment

0 Comments