Waliofariki watajwa ni kutoka ITV, Uhuru Digital, maafisa habari

NA GODFREY NNKO

CHANZO cha habari cha kuaminika kutoka eneo la tukio kimeieleza DIRAMAKINI BLOG kuwa,waandishi wa habari waliofariki katika ajali hiyo ni wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini jijini Mwanza.
Vyombo hivyo ni pamoja na ITV Tanzania, Uhuru Digital, Afisa Habari kwa upande wa mkoa na yule wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe na wengineo.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili likiwemo la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara baada ya kugongana uso kwa uso leo Janauri 11, 2022.

Tayari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, ameahirisha ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali hiyo.

DIRAMAKINI BLOG imeelezwa kuwa, viongozi wa Serikali na waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza walikuwa wanajiandaa kuelekea eneo la tukio kwa taarifa zaidi.

Kutoka Mwanza Press Club

"Ndugu  waandishi wa habari na wadau wa habari , asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.

Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua marehemu.

Waliofariki ni 

1.Husna Milanzi - ITV

2.Johari Shani - Uhuru Digital

3.Antony Chuwa - Freelancer 

4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza

5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi

1.Tunu Heman - Freelancer

2 Vany Charles - Icon TV

Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.

Taarifa nyingine za uratibu kuhusu msiba tutawajuza.

Mwanza Press Club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.

Kazi ya Bwana haina makosa, jina.lake lihidimiwe.

Edwin Soko

Mwenyekiti

Mwanza Press Club

11.01.2022

Post a Comment

0 Comments