Waziri wa Afya atoa maelekezo kwa hospitali za rufaa za mikoa nchini

NA MWANDISHI MAALUM-WA

HOSPITALI za rufaa za mikoa nchini zimetakiwa kuboresha huduma za afya pamoja na kuwa na mawazo mapana katika uboreshaji wa miundombinu ya hospitali hizo ili kuweza kuisaidia na kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumzia na watumishi.

Hayo yamesemwa leo Januari 18,2022 na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wafanyakazi wa idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na kufanya mapitio ya idara mbalimbali zilizopo kwenye wizara hiyo.
Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na watumishi wa idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kuongea na idara mbalimbali Kwenye wizara hiyo.

Mhe. Ummy amesema, ili kuonesha kweli idara ya tiba ndio inayobeba wizara hiyo hamna budi kuboresha huduma hizo ili zilingane na mahitaji ya wananchi, kwani wananchi wanaziamini hospitali za umma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi akiongea na watumishi wa Idara ya Tiba.

“Tunatakiwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya ni mzuri, hivyo ni wakati wa kuangalia changamoto na kuziboresha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wanafika kwenye vituo vyetu kupata huduma," amesema Mheshimiwa Ummy.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Aifello Sichalwe akiongea jambo wakati wa kikao kazi hicho.

Aidha, Waziri huyo ameitaka idara hiyo kufanya upya mapitio ya miongozo ya utoaji huduma ili kufanya huduma zinazotolewa kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa zinakuwa bora na zenye manufaa kwa wananchi vilevile miongozo hiyo iweze kuunganisha vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hata hivyo, Waziri Ummy amewataka watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kama timu na endapo kuna changamoto ni vyema zikajadiliwa kwa pamoja ili kwenda kwa pamoja katika kuboresha huduma za afya nchini

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news