BREAKING NEWS: Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 4, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Khamis Adam Khamis kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, ndugu Khamis ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Abdalla Ali Mwinyigogo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba. Kabla ya uteuzi huo,ndugu Abdalla alikuwa Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Ardhi na Maenbdeleo ya Makaazi.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Khadija Bakari Juma kuwa mwenyekiti wa Baraza la Elimu. Ndugu Khdadija kabla ya uteuzi alikuwa mstaafu katika utumishi wa umma.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Fatma Mode Ramadhan kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Kabla ya uteuzi huo,ndugu Fatma alikuwa Afisa wa Idara ya Maandalizi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Othman Omar Othman kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, ndugu Othman alikuwa Afisa Mwandamizi Idara ya Mipango Sera na Utafiti katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua ndugu Abdalla Agmed Mussa kuwa Mkurugenzi wa Idara ta Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Kabla ya uteuzi huo, ndugu Abdalla alikuwa mwalimu katika Skuli ya Haile Salasie.

Saba, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Abdalla Mohammed Mussa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Elimu Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, ndugu Abdalla alikuwa Afisa Mwandamizi Taasisi ya Elimu Zanzibar.

Wengine walioteuliwa ni,


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news