Radi yaua saba wakiwa shambani,14 wajeruhiwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WATU saba wameripotiwa kufariki katika matukio mawili tofauti yaliyotokea katika Kijiji cha Milundikwa kKta ya Nkandasi wilayani Nkasi pamoja na Kijiji cha Luwa Kata ya Ntendo Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo kwa kupigwa na radi.
Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, William Mwampaghale amesema kuwa, katika tukio la kwanza lililotokea Februari 26, 2022 majira ya saa 9 mchana Kijiji cha Nkandasi wilayani Nkasi ambapo watu watano waliokuwa wakifanya kibarua cha kupanda maharage shambani walikufa papo hapo huku 14 kati yao walijeruhiwa baada ya kupigwa radi wakiwa wamejikinga kwenye kijumba kidogo shambani humo.

Amesema kuwa, watu hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao, baada ya kuona mvua imeanza kunyesha waliacha kupanda maharage na kuamua kukimbilia kwenye kijumba kidogo kilichopo shambani hapo kwa ajili ya kujikinga mvua.

Kamanda amesema kuwa, wakiwa wamekaa humo ghafla radi ilipiga kijumba hicho na kusababisha vifo hivyo na kujeruhi wengine waliokuwa wamejikinga mvua katika nyumba hiyo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkandasi, Given Kisantola amesema kuwa waliofariki ni wanaume watatu na wanawake wawili na majeruhi walikimbizwa katika zahanati ya jeshi Milundikwa kwa ajili ya matibabu na wengi wao wanaendelea vizuri huku wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Yusuph Mbalamwezi (24),Leonard Wayomba (21)Flansisco Kangama, Fazil Wayomba (24), Shukuru Mutayagwa (28) na mtoto Abinet Kazumba (8)

Majeruhi katika tukio hilo ni Veronica Saanane(27), Fobi Mbonile(28) Solostina Sokoni (39), Edina Noel (39) Getruda Mwananjela (34) mtoto Tatu Miyula (10) Teddy Wazamani (37),Mary Kauzeni (18)Daniel Kamilembe (19), Lenatha Chakula (51),Magreth Savery (40),Retisiya Fataki (38) na Veronica Swaila (27)

Kamanda Mwampaghale alisema katika tukio la pili lililotokea siku hiyo hiyo mwanaume mmoja ambaye jina lake halijajulikana mkazi wa kijiji cha Luwa kata ya Ndendo Manispaa ya Sumbawanga amekufa papo hapo yeye na mtoto wake baada ya kupigwa radi wakiwa shambani wanalima.

Aidha Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi wanapokuwa wanafanya shughuli mbalimbali kuchukua tahadhari kwa kuacha pindi wanapoona kuna dalili za mvua kuanza kunyesha kwani nyakati hizi za masika ni hatari kutokana na kuwepo kwa radi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news