Rais Samia kuzindua miradi ya maendeleo mkoani Mara

NA FRESHA KINASA

MKUU wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ally Hapi amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwasili mkoani hapa Februari 4, 2022 kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 45 za kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yatakayofanyika Februari 5, 2022 Mjini Musoma.

Pia amesema, Mheshimiwa Rais atafanya ziara ya kiserikali ya kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 126 kuanzia Februari 6 na 7, 2022 ambapo pia atazungumza na wananchi. 
Ameyasema hayo leo Februari Mosi, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Mjini Musoma ambapo amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Mara kujitokeza kwa wingi katika sherehe za miaka 45 zitakazofanyika Mjini Musoma na wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Butiama, Musoma na Bunda.

Amesisitiza kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuimarisha usalama kuwezesha ugeni wote unafanyika kwa amani na usalama, kwani macho ya Dunia amesema yapo mkoani Mara kuona mambo yote yanafanyika kwa ufanisi mkubwa. 

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atawasili mkoani Mara, Februari 4, 2022 ambapo Februari 5, 2022 atashiriki maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ambayo kitaifa yanafanyikia Mjini Musoma na baada ya hapo atafanya ziara ya kiserikali ya kuzindua miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji wa Mugango-Kiabakari, Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo la Kwangwa, ataweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Bunda na kuongea na Wananchi wa Musoma Vijijini, Manispaa ya Musoma, kutembelea kaburi la Baba wa Taifa huko Butiama,"amesema Mheshimiwa Hapi.

Amehimiza wakazi wa Mkoa wa Mara kumpokea kwa bashasha na shangwe wakati akiwasili mkoani humo kwani ni heshima kubwa na ya kipekee kwa wakazi wa Mkoa wa Mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news