Wapongezwa kwa kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa ufanisi Mihambwe

NA MWANDISHI MAALUM

WAUGUZI katika Zahanati ya Mihambwe iliyopo Kata ya Mihambwe Tarafa ya Mihambwe mkoani Mtwara wamepongezwa kwa kuongoza wa kwanza kiwilaya kwa wingi wa utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 kwa watu.
Hayo yamebainishwa Februari 1, 2022 wakati wa ziara iliyofanywa na Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu kwenye Zahanati ya Mihambwe ambaye alienda kuwapongeza Wauguzi na kusikiliza changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzipatia utatuzi.

"Kwanza Serikali tunawapongeza kwa utoaji wa huduma bora nyakati zote. Pili sio kwa umuhimu, Serikali tunawapongeza kwa uongozaji kiwilaya uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 ambapo Zahanati ya Mihambwe mmekuwa wa kwanza kiwilaya, mmechanja jumla ya Watu 1,405 na anayefuata amechanja watu 342. Hongereni sana, nawasihi muendelee kuwa bora zaidi. 

"Pia nawapongeza wananchi wa Tarafa ya Mihambwe kwa kuitikia na kuunga mkono kivitendo wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kuchanja chanjo ya Uviko-19 kwa hiyari yao,"amesema Afisa Tarafa huyo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Dkt. Merkezedek Liyama alishukuru kwa kuona mchango wa utendaji kazi wao umeonekana na kuthaminiwa.

"Sisi tunashukuru kwa kuyaona yale tunayoyafanya na tunaahidi kuendelea kupambana kutoa huduma bora pasipo kuchoka," amesema Dkt.Liyama.
Tarafa ya Mihambwe ina Zahanati 5 na Kituo cha Afya kimoja ambacho kipo hatua ya ukamilishwaji kujengwa tayari kuanza huduma.

Katika ziara hiyo ya kutembelea Zahanati ya Mihambwe, Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Mihambwe na kuhaidi kutatua changamoto zinazowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news