Waziri Bashungwa aweka wazi umuhimu wa Kalenda ya Utekelezaji wa Mitaala ya Shule

NA MWANDISHI MAALUM-OR TAMISEMI 

KALENDA ya Utekelezaji wa Mitaala ya Shule za Msingi na Sekondari imelenga kuhakikisha utekelezaji wa mitaala unazingatia taratibu zote za ufundishaji na ujifunzaji.

Sambamba na kuhakikisha kunakuwepo na ulinganifu na usawa wa ukamilishaji katika utekelezaji wa mitaala kwa ngazi husika katika maeneo yote nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati akijibu hoja katika semina ya wabunge juu ya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya elimu ya awali, msingi na sekondari iliyofanyika bungeni jijini Dodoma leo Februari 14, 2021.

Waziri Bashungwa amesema, kalenda hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo itawezesha wasimamizi wa elimu kufanya usimamizi, ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mitaala kwa urahisi.

Pia kuwapa fursa wanafunzi wanaohama kutopoteza au kurudia baadhi ya mada ambazo zingeweza kuwa zimeshafundishwa kabla au baada. 

Aidha, kalenda ya utekelezaji wa mitaala imeandaliwa kawa kuzingatia muhtasari wa masomo na idadi ya wiki ya masomo katika mwaka ili kuweka mpangilio na mtiririko wa ufundishaji na umahiri na kupangilia idadi ya vipindi kwa kila mahiri bila kuathiri idadi.

Wakati huo huo, wabunge wamepata fursa ya kuelezwa umuhimu wa kalenda za utekelezaji wa mtaala ambao ni kuwaongoza walimu wa somo kuandaa mpango wa ufundishaji, kuwawezesha wanafunzi kukuza umahiri uliobainishwa kwenye mtaala kwa kuzingatia muda ulioelekezea katika kalenda.

Vile vile, kalenda za utekelezaji wa mtaala itawaongoza walimu kufanya upimaji wa ufundishaji kwa kuzingatia maudhui yaliyoelekezwa kufundishwa katika kalenda ya mwaka na kuwaongoza wapimaji wa watahini kuandaa mitiani inayoendana na mtiririko wa ufundishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news