Yanga SC,Mbeya City ni 'Mwakasare' leo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

YANGA SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Ni mtanange uliopigwa leo Februari 5,2022 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga SC inafikisha alama 36 na kuendelea kuongoza ligi kwa alama nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 14.

Mbeya City yenyewe inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa alama moja na Azam FC.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu NBC leo, Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Erick Mwijage dakika ya 20 na 73, wakati la Coastal Union limefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 54.

Kagera Sugar inafikisha alama 19 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union inabaki na alama zake 17 katika nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 14.

Nayo KMC imelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United katika dimba la Azam Complex, Chamazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

KMC inafikisha alama 16 katika nafasi ya 10 na Biashara United inafikisha alama 12 katika nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 14.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news