Biashara United yatembeza kichapo kwa Tanzania Prisons

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WANAJESHI wa mpakani ambao ni timu ya Biashara United wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Mtanange uliopigwa leo Machi 15, 2022 katika dimba la Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara.

Mabao ya Biashara United ambao walikuwa wenyeji yamefungwa na Deogratius Mafie dakika ya 26 na 34.

Aidha, kwa upande wa Prisons Tanzania, bao limefungwa na Ezekiah Mwashindilindi dakika ya 68.

Biashara United kwa matokeo hayo inafikisha alama 19 na kusogea nafasi ya 13, wakati Prisons inaendelea kushika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na alama 13.

Ni baada ya wote kucheza mechi 18 katika ligi hiyo ambayo ina mvuto wa kipekee kutokana na kila mmoja kutamani kuwa katika nafasi nzuri ili kuweza kutwaa fungu nono mwisho wa siku.

Post a Comment

0 Comments