Simba SC:Kila tutakayekutana naye ni halali yetu,mtupishe

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

NI wazi kuwa, Klabu ya Simba imedhamiria kusonga mbele katika michuano inayowakabili ikiwemo ya Kitaifa na Kimataifa ambapo kwa sasa wamejichimbia huku wakipiga zoezi kali.Wimbo wao ukiwa kila watakaye kutana naye ni halali yao.
Mazoezi hayo yanakuja baada ya Pape Ousmane Sakho kupitia mtanange wa hivi karibuni katika dakika ya 44 kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Ni katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Winga huyo Msenegal alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Mnyarwanda, Meddie Kagere.
Kwa ushindi huo, Simba ilifikisha alama saba na kupanda kileleni mwa kundi hilo, ikiizidi alama moja Berkane. 

Wakati huo huo, leo Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na ushindi na 2-1 kwenye mchezo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiasso kwenye dimba la Mo Simba Arena huko Bunju jijini Dar es Salaam.

Simon Msuva ndiye aliyeipatia Cambiasso bao huku upande wa Simba SC yakifungwa na Erasto Nyoni na Clatous Chama.

Post a Comment

0 Comments