DC Mboneko akagua miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA Shinyanga

NA MARCO MADUHU

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amefanya ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ambayo inatekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto) akifungua Maji Bombani katika kituo cha kuchotea maji kwenye Shule ya Msingi Masengwa wilayani Shinyanga, (katikati) ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga, Edward Ngelela na (wapili kutoka kulia) ni Meneja wa RUWASA, Wilaya ya Shinyanga, Emmael Nkopi.

Mboneko amefanya ziara hiyo Machi 16,2022, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani, ambacho kilele chake ni Machi 22 mwaka huu, na alikuwa ameambatana viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na chama cha mapinduzi CCM wilayani humo.

Alisema katika miradi ya maji ambayo ameitembelea, amekuta imeshakamilika kwa asilimia kubwa, na kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa maji safi na salama katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga, na kupongeza kazi kubwa ambayo wanaifanya Ruwasa ya utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, akizungumza kwenye ziara hiyo ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi, na leo nimeona kazi ambayo imefanyika ambapo miradi inataoa maji, na katika maadhimisho ya wiki ya maji hapa Shinyanga sisi ni kufungulia maji kwenye mabomba tu na kumtua ndoo kichwani mwanamke, na kumuondolea adha ya kufuata maji umbali mrefu," alisema Mboneko.
Mwanamke Ester Jilala mkazi wa kijiji cha Ibubu Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga akielezea furaha ya kupata maji safi na salama kijijini humo.
"Katika miradi hii ya maji ambayo imetekelezwa na wasihi wananchi muitunze miundombinu yake na kutoiharibu, ili idumu kwa muda mrefu kuwa hudumia na kuendelea kupata maji safi na salama," aliongeza.

Aidha, alizionya kamati za maji kuwa pesa ambazo watakuwa wakizikusanya kwenye vituo vya kuchotea maji, wazipeleke benki kwenye akaunti husika na siyo kuzifanyia ubadhilifu.
Diwani wa Masengwa Nicodemas Simon, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Diwani wa Iselamagazi Isack Sengerema, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.

Pia, aliwataka watu ambao wanasimamia kuuza maji kwenye vituo, wawepo muda wote na siyo kuanza kutafutwa, ili wananchi wafurahie huduma hiyo ya maji safi na salama na kuacha kutumia maji yasiyofaa.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Vijijini, Edward Ngelela, amepongeza utekelezaji wa miradi hiyo ya maji, na kubainisha kuwa huo ndiyo utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa vitendo.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Mwanafunzi Betha Emmanuel ambaye anasma shule ya msingi Masengwa, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA)wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani, ambapo shule hiyo nayo ni wanufaika wakuu wa mradi wa maji safi na salama shuleni hapo.

Nao baadhi ya akina mama akiwemo Rebeka Mpuya na Jesca Masanja, walisema huduma hiyo ya maji kuwa karibu, imewaondolea changamoto ya kufuata maji umbali mrefu, na hawataugua tena magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Maji Vijijni (RUWASA) wilayani Shinyanga, Emmael Nkopi, alisema asilimia kubwa ya miradi ya maji ambayo wanaitekeleza wilayani humo umeshakamilika, na mingine kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news